PROF. MONELA APEWA NGAO YA HESHIMA

ngaomonela

Na Halima Katala Mbozi

Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii  kutoka Chuo  Kikuu cha Sokoine  cha Kilimo(SUA) kwa kutambua na kuthamini mchango ambao  ameutoa  katika kipindi cha  uongozi wake aliyekuwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Gerald  Monela wamemzawadia Ngao ya  shukrani  kwa ajili ya kumpongeza.

Akizungumza katika hafla  fupi iliyoandaliwa chuoni hapo Rasi wa ndaki  ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy amesema dhumuni la kuandaa  hafla hiyo ni kumpongeza na kumkabidhi Ngao ya shukrani kwa kipindi chote cha miaka 10 alichoongoza  akiwa Makamu wa Mkuu wa Chuo (SUA).

ngaomonela

Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy akimkabidhi  Tuzo ya shukrani aliyekuwa Mkamu wa Mkuu wa Chuo SUA Prof. Gerald Monela, kulia ni  Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho upande Taaluma Prof. Peter Gillah.( Picha na Halima Katala Mbozi )

Prof. Kessy amesema kuwa wao kama Ndaki wameamua kumkabidhi zawadi hiyo ikiwa ni  ishara ya kumpongeza na  iwe kumbukumbu  kwake ya shukrani kwa  kile alichokifanya kipindi chote cha uongozi wake.

ngaomonela1

Kwa upande wake Prof. Gerald Monela ametoa shukrani zake za dhati kwa  wafanyakazi wote wa Ndaki  ya Misitu, Wanyamapori na Utalii  kwa ushirikiano wao  waliouonesha kwake katika kipindi chote alichokuwa nao na kuwashukuru  kwa kuendelea kushirikiana nae katika shida na raha alizopitia na kuwaomba waendelee na moyo huo.

ngaomonela2

Gerald Monela akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Tuzo ya shukrani baada ya kumaliza Uongozi wake, kutoka kulia ni Naibu Makamu mkuu wa Chuo upande wa Taaluma na kutoka kushoto ni Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy (Picha na Halima Katala Mbozi)

Aidha Prof. Monela amewataka waadhiri wote ambao ni wazoefu kuwasaidia wale ambao hawana uzoefu wa kutosha ndani na nje ya Ndaki zote za chuo ili kuongeza ujuzi na maarifa katika utendaji na ubunifu wa Teknolojia mpya.

Related Posts