Nafasi za kazi : Afisa Miti (nafasi 200)

KILOLO, IRINGA, MUFINDI, NJOMBE, WANGING’OMBE MBEYA VIJIJINI, MBOZI, SONGWE

WAJIBU NA MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kusimamia uandikishaji wa wakulima waliokidhi vigezo vya mradi
  • Kukusanya na na kutuma taarifa za Marejesho za Wakulima
  • Kutoa Mrejesho wa Maendeleo na changamoto kwa Msimamizi
  • Kushirikiana na wakulima katika kufanikisha Utekelezaji wa Mafanikio ya Mradi

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe na elimu ya Sekondari, Astashahada (Certificate) katika Kilimo, Mazingira, Maendeleo ya Jamii au Maeneo yanayohusiana.
  • Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana kwa Kiswahili fasaha.
  • Awe na ujuzi katika masuala ya Teknolojia (Matumizi ya Smartphone au Tablet) na ukusanyaji wa data.
  • Awe na uzoefu wa kufanya kazi na wakulima, hasa katika maeneo ya vijijini.
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya kijijini na kusafiri umbali mrefu.
  • Awe na viambatanisho mhimu vifuatavyo. Nakala ya kitambulisho au namba ya NIDA, Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha mpiga kura Nakala za vyeti vya elimu (kuanzia kidato cha nne, astashahada nk.)

JINSI YA KUOMBA:

  • Hakikisha maombi yako yanaonyesha Mahali ulipo kwa sasa, Wilaya unayoomba kufanyia kazi, Vijiji angalau 3 unavyopendelea kufanya kazi, na Ueleze kama uko tayari kufanya kazi katika vijiji vingine tofauti na ulivyo pendekeza. Tazama hapa Orodha ya Vijiji vyenye nafasi za Kazi
  • Wasilisha maombi Kwa Njia ya Mtandaoni (Online), Tuma barua yako ya maombi na wasifu (CV) kwa njia ya mtandao kupitia tovuti hi (https://bit.ly/fomumtandao) ya mtandao. AU
  • Tuma Maombi (Barua yako ya Maombi na Wasifu (CV) kwenye Ofisi zetu au Maduka ya OAF yaliyopo mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya & Songwe. Vijiji vya Nafasi za Afisa Miti vinapatikana https://bit.ly/vijijivyote

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kazi ni: 22th September, 2024

Kumbuka

Kwa changamoto yoyote utakayo ipata piga simu au tuma ujumbe kwa ufafanuzi zaidi kwa namba zifuatazo; MBEYA, MBOZI & SONGWE: 0769819461

KILOLO, IRINGA, MUFINDI: 0757242199

NJOMBE & WANGING OMBE: 0764079771

OMBA

 

Kama unatokea sehemu tofauti na vijiji ambavyo nafasi za Afisa Miti Zinahitajika, One Acre Fund haitagharamikia gharama zozote za uhamisho.

Nafasi za Kazi_ Afisa Miti (200) - OAF (1)

Global Biodiversity Information Facility

Related Posts