Mwongozo wa uvunaji katika misitu ya hifadhi ya vijiji

Tafsiri rahisi ya mwongozo wa uvunaji katika misitu ya hifadhi ya vijiji umetafsiriwa kutoka kwenye kitabu kilichotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013. Kutokana na mwongozo huo kuandaliwa katika lugha ya kiingereza, Idara ya Misitu na Nyuki kwa kushirikiana na Kampeni ya Mama Misitu imeratibu utengenezaji wa tafsiri rahisi ya mwongozo wa uvunaji katika misitu ya hifadhi ya vijiji ili kuongeza ushiriki wa jamii hasa za vijijini katika kutekeleza mipango ya uvunaji endelevu katika maeneo yao.

Kijitabu cha mwongozo wa uvunaji katika misitu ya hifadhi ya vijiji kitasaidia kamati za maliasili, Serikali za vijiji, Halmashauri za Wilaya, Asasi za kiraia, wafanyabiashara wa mazao ya misitu na wananchi kwa ujumla kufahamu kazi na majukumu yao katika kuwezesha uvunaji endelevu na wenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Idara ya Misitu na Nyuki inatoa shukrani kwa wadau wote walioshiriki na kutoa maoni yao katika uandaaji na uboreshaji wa tafsiri hii rahisi ya mwongozo wa uvunaji katika misitu ya hifadhi ya vijiji. Kipekee, tunatoa shukrani kwa Kampeni ya Mama Misitu kwa kuwezesha uchapishaji wa kijitabu hiki.

guidelines_-_uvunaji_v2

Global Biodiversity Information Facility

Related Posts