Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anapenda kuwaarifu Waombaji wa nafasi mbalimbali za kazi zilizotangazwa tarehe 08.06.2023 kwamba usaili wa nafasi hizo umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 01 Agosti, 2023 hadi 02 Agosti, 2023 Katika Kampasi ya Edward Moringe Mjini Morogoro. Waombaji watakaofaulu katika mchakato huo watapangiwa vituo vya kazi na Menejimenti ya Chuo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili huo ni wale waliokidhi vigezo kutokana na sifa zilizoainishwa katika tangazo la kazi lilitolewa, na wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika tarehe 01 Agosti, 2023 hadi 02 Agosti, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika vimeainishwa kwa kila Kada/kundi.
- Kila Msailiwa anapaswa kufika na moja kati ya vitambulisho vifuatavyo:- Kitambulisho cha Mkazi, kazi, Mpiga kura, Uraia au Hati ya Kusafiria.
- Kila Msailiwa anapaswa kufika na VYETI HALISI, vya kuzaliwa, Sekondari (kidato cha IV, VI), Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. Msailiwa yeyote atakayewasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) badala ya vyeti halisi,
HATARUHUSIWA KUENDELEA NA MCHAKATO USAILI. iv. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kila Msailiwa aliyesoma nje ya Tanzania afike na vyeti vya uthibitisho (ithibati) vilivyohakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au
NECTA) vii. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo vilivyoainishwa katika tangazo la kazi. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia vigezoi vya tangazo husika.
- Kila Msailiwa ambaye taaluma yake inahitaji usajili wa Bodi za Kitaaluma na sifa hiyo, anapaswa kufika na cheti/vyeti Halisi vya Usajili
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
- Msailiwa haruhusiwi kuja na simu au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la usaili.