Prof. Ngaga apewa ngao ya heshima na Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii

Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kutambua na kuthamini mchango ambao ameutoa  katika kipindi cha  uongozi wake aliyekuwa Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Yonika Ngaga wamemzawadia Ngao ya  heshima  kwa ajili ya kumpongeza na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine ya kazi.

Akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa chuoni hapo Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy amesema dhumuni la kuandaa hafla hiyo ni kumpongeza na kumkabidhi Ngao ya heshima na shukrani kwa kipindi chote cha miaka 4 alichoongoza akiwa Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.

Prof.Kessy

Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy akitoa pongezi kwa Prof. Ngaga

Prof Gillah akitoa neno la shukurani CFWTjpg

Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Peter Gillah akitoa neno la kumpongeza Prof. Ngaga baada ya kumaliza vizuri kipindi chake cha uongozi 

 

Prof Ishengoma akitoa neno la shukrani CFWT

Prof. Ishengoma akitoa neno la pongezi kwa niaba ya wafanyakazi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kwa Prof. Ngaga

 

Prof Abdallah akitoa salam za pongezi kwa Prof. Ngaga

Prof Abdallah akitoa salam za pongezi kwa Prof. Ngaga

 

Prof. Ngaga akiwashukuru wafanyakazi wote wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori na utalii kwa ukarimu wao

Prof. Ngaga akiwashukuru wafanyakazi wote wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kwa ukarimu wao

Prof. Ngaga

Prof. Ngaga apewa ngao ya heshima

Prof. Ngaga akiwa na ngao yake aliyotunukiwa na Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii

Picha ya pamoja