Tarehe 5 Juni 2024, siku ya mazingira duniani, tunawakumbusha watanzania kuhifadhi mazingira na kujiongezea kipato kwa kuwasajili miradi yao ya kaboni. Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni, NCMC, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), inatambua umuhimu wa utunzaji mazingira na faida za biashara ya kaboni. Kwa sababu hiyo, NCMC inatangaza kazi za kuhifadhi mazingira na kujiongezea kipato kwa kuwasajili miradi ya kaboni.
Kazi hii inatakiwa kufanyika kwa kushirikiana na idara za mifumo ikolojia, uhifadhi, tathmini, na usimamizi wa rasilimali za misitu. Hii itasaidia kuweka mazingira salama na kukuza biashara ya kaboni katika enzi hizi ambazo suala la utunzaji mazingira limekua likipewa kipaombele zaidi ili kukabilina na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Tovuti ya NCMC pamoja na zile za idara za ndaki ya usimamizi wa misitu, wanyamapori na utalii ambazo ni tovuti ya idara ya Uchumi wa Misitu na Mazingira ikishirikiana na idara ya Mifumo Ikolojia na Uhifadhi pamoja na idara ya Tathmini na Usimamizi wa Rasilimali za Misitu zinatoa elimu bobevu kuhusu utunzaji wa misitu na faida za biashara ya kaboni. Watanzania wanatakiwa kutembelea tovuti hizi ili kujifunza zaidi kuhusu miradi ya kaboni na jinsi ya kuhifadhi mazingira.