Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kutambua na kuthamini mchango ambao ameutoa katika kipindi cha uongozi wake aliyekuwa Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Yonika Ngaga wamemzawadia Ngao ya heshima kwa ajili ya kumpongeza na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine ya kazi.
Akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa chuoni hapo Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy amesema dhumuni la kuandaa hafla hiyo ni kumpongeza na kumkabidhi Ngao ya heshima na shukrani kwa kipindi chote cha miaka 4 alichoongoza akiwa Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. John Kessy akitoa pongezi kwa Prof. Ngaga
Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Peter Gillah akitoa neno la kumpongeza Prof. Ngaga baada ya kumaliza vizuri kipindi chake cha uongozi
Prof. Ishengoma akitoa neno la pongezi kwa niaba ya wafanyakazi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kwa Prof. Ngaga
Prof Abdallah akitoa salam za pongezi kwa Prof. Ngaga
Prof. Ngaga akiwashukuru wafanyakazi wote wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii kwa ukarimu wao
Prof. Ngaga akiwa na ngao yake aliyotunukiwa na Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii