Kwanini tujisumbue? Vyema, kwanza kabisa, ni kwa sababu kutazama nyani na kuorodhesha nyani uliowaona ni mambo la kufurahisha. Sisi ambao tuna mahaba na Wanyama hawa kama ilivyo kwa watazamaji wa ndege kwa ndege wao, ki ukweli tunafurahia sana tunapowaona nyani (monkeys), nyani wakubwa (apes), Komba bukini, lorises, Komba (galagos), potto na tarsiers katika mazingira yao ya asili, na tunawataka ninyi pia muwe na msisimko juu ya Wanyama hawa, lakini kwa kweli kuna zaidi kuliko burudani tu.