Kilio cha dhiki kutoka nyikani

Uwindaji Haramu wa wanyamapori ni tatizo kubwa linalotishia uwepo wenyewe wa spishi kadhaa za wanyama nchini Tanzania. Kutega mitego ni njia kuu ya uwindaji haramu wa wanyama inayofanywa kwa kutumia nyavu zilizoundwa kwa vipande vya waya vilivyojengwa kwenye duara na kufungwa chini, na kuwekwa katika eneo lenye shughuli kubwa za wanyama lengo kuu likiwa ni kuua wanyamapori kwa sababu kadhaa ikiwemo nyama ya porini na shughuri zingine za kiuchumi na kitamaduni. katika uwindaji huo wanyama kadhaa wakubwa kwa wadogo wamekua wakilengwa; Simba, Nyati, swala na hata Faru wamekua miongoni mwa wanyama wanaoathirika na aina hii ya uwindaji haramu Tanzania.

katika makala iliyoandikwa hivi karibuni na mwandishi na mwanaharakati wa uhifadhi aliyebobea katika maswala ya usimamizi na uhifadhi wanyamapori ndugu Hillary Mrosso inaonyesha ni kwa jinsi gani tatizo la uwindaji haramu kwa kutumia nyaya ngumu (Snare) limechangia kwa kiasi kikubwa kupungua idadi ya simba katika hifadhi za Taifa Tanzania.

Ndugu Hillary Mrosso akionesha jinsi mitego ya waya inavyo nasa wanyama

Bofya hapa kusoma zaidihttps://wildlifetanzania.co.tz/sauti-ya-dhiki-kutoka-mbugani/

Related Posts